Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa
Amewataka wakandarasi hao kuwa na mkakati wa kumaliza ujenzi wa miradi hiyo hadi kufikia mwishoni mwa Oktoba mwaka huu
Akizungumza katika vikao kazi baina ya uongozi wa Tume na wakandarasi hao mkaoni humo Mndolwa amesisitiza wakandarasi hao wafanye kazi usiku na mchana kumaliza mradi kwa wakati.
Wakandarasi wanaojenga mradi wa Mkombozi lot I na lot II unaofanywa na kampuni ya ndani ya Cimfix & engineering, sambamba na ujenzi wa mradi Mkombozi lot III na lot IV unajengwa na kampuni ya CRJE Engineering kutoka China
Mndolwa pia aliongoza kikao kazi baina ya Tume na Mkandarasi ujenzi wa Mkombozi M/S Cimfix& Engineering Co Ltd kilicho fanyika katika kambi ya Mkandarasi anayetekeleza mradi wa Mkombozi lot I na II Mkoani Iringa.