''Njooni kwa wingi uwanja wa Uhuru'' - RC Dar

Jumamosi , 25th Jul , 2020

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amewaomba wakazi wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru kuanzia kesho Julai 26, 2020 katika kuaga mwili wa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge

Amesema hayo leo Julai 25, 2020 hii wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika uwanja wa taifa kuuangalia hatua zinazoendelea ambapo amesema wamejipanga vizuri katika kuhakikisha usalama kwa raia unakuwepo.

“Nataka kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa  Dar es salaam hali ya usalama ni nzuri, na tumejipanga vizuri, vyombo vyetu vimekaa vizuri kwahiyo tusiwe na wasiwasi tujitokeze kwa wingi nakuaga kutakuwa kuanzia asubuhi hadi jioni”.

Aidha Mkuu wa mkoa huyo amewaomba wale ambao hawatapata nafasi yakuingia uwanjani siku ya kesho wawepo barabarani mara watakapopatiwa ratiba juu ya njia watayopitia ili waweze kumuaga kutokana na sehemu waliokuwepo.