Ijumaa , 3rd Mar , 2023

Mrakibu wa Magereza Tanzania ambaye pia ni Boharia katika gereza la wafungwa na mahabusu Segerea amesema licha bajeti inayowekwa kuwahudumia wafungwa bado haitoshelezi hivyo kuwataka na kuwasifu wadau wanaojitokeza kupeleka vitu katika Magereza hiyo.

Wito huo umetolewa mara naada ya kupokea msaada wa vitu kutoka kwa wanawake kutoka mfuko wa taifa wa hifadhi kwa jamii NSSF ambapo kila tarehe 3 mwezi wa watu wanawake kutoka maeneo mbali mbali huanza kusherehekea mwezi huo kwa matukio mbalimbali ambapo hii leo wanawake kutoka mfuko a hifadhi za jamaii NSSF wametembelea na kutoa misaaada kwa wafungwa wanawake katika gereza la segerea ikiwa ni ishara ya upendo kwa wanawake wenzao ambao wanatumikia vifungo vyao katika gereza hilo

Kwa mujibu wa Mrakibu wa Magereza na Boharia kutoka mahabusu hiyo ya Segerea amesema walioko ndani ni watu kama wengine na wanahitaji mahitaji kama watu wengine hivyo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia huku akitaja baadhi ya mahitaji muhimu kama sabuni,yeboyebo,dawa za meno na vitu vingine