Jumatano , 4th Mei , 2016

Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya magari ya kifahari nchini Tanzania, yamekuwa yakiharibika na kufa muda mfupi tangu yanunuliwe kutokana na wamiliki wake kununu mafuta na vilainishi visivyoendana na mahitaji ya injini zake.

Afisa kutoka kampuni ya AGL ambao ni watengenezaji wa vilainishi na mafuta aina ya Atlantic, Bi. Sarah Heri mesema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati EATV ilipotaka kufahamu athari zinazotokana na matumizi ya vilainishi visivyokidhi viwango ambavyo vimekuwa vikiuzwa katika maduka sehemu mbali mbali nchini.

"Magari mengi ya kifahari nchini yamekuwa hayatumii mafuta na vilainishi vinavyoendana na aina za magari hayo, hii ndio sababu pekee ya magari hayo kufa na kuharibika kabla ya muda, kitaalamu magari hayo yanatumia mafuta aina ya 0W-20 ambayo sisi ndio waagizaji pekee wa mafuta hayo hapa nchini," amesema Bi. Sarah.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo hapa nchini Bw. Nassif Bachaalan amewatahadharisha wenye magari kuacha kununua bidhaa kwa kigezo cha unafuu wa bei na badala yake waangalie mafuta na vilainishi vinavyoendana na vipimo vya kitaalamu vya magari husika.

"Ajabu ya watumiaji wa magari hapa nchini ni kwamba mara nyingi wamekuwa wakiulizia bei badala ya ubora wa mafuta...hii ni hatari kwani ni rahisi kubadili aina ya mafuta lakini sio rahisi kubadili injini ya gari, ni bora waanze sasa kununua mafuta na vilainishi halisi vya Atlantic badala ya kukimbilia unafuu ambao mara nyingi umekuwa ukiwagharimu," amesema Bw. Bachaalan.