Alhamisi , 6th Oct , 2022

Vijana 40 wanaotuhumiwa kuwa ni panya road, wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha, kuvunja nyumba na kujeruhi watu maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, ambapo wote kwa pamoja walikana mashtaka hayo.

Baadhi ya watuhumiwa wa panya road wakiwa mahakamani

Watuhumiwa hao walitenda makosa hayo Septemba 19 hadi 21 mwaka huu, maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo walivunja nyumba usiku na walipora mali baada ya kuwajeruhi wananchi kwa kutumia silaha za jadi ambazo ni mapanga, nondo, visu na kukimbia.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama hiyo mbele ya Mahakimu watatu, Hakimu Mkazi Glory Nkwera, Fadhili Luvinga, Rehema Liana, na kwamba kesi yao imeahirishwa hadi Oktoba 19, 2022.