
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini
Kauli hiyo imetolewa hii leo Mei 10, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini, wakati akijibu swali la mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, lililohusu ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya vikundi vya Panya road vinavyopora na kujeruhi watu.
"Tumeaahidi kushughulika na vijana hawa wakitu-beep sisi tutawapigia, kwahiyo kwa tahadhari hiyo tunaomba watafute kazi nyingine ya kufanya badala ya uhalifu wanaoufanya dhidi ya binadamu hatutawavumilia," amesema Naibu Waziri