Ijumaa , 6th Jan , 2023

Mwili wa Papa  Benedict wa 16 umezikwa katika eneo la kanisa la St. Peter huku ibada ikiongozwa na Baba Mtakatifu Francis

Baba Mtakatifu Francis Januari 5/2023 aliwaongoza  maelfu ya waombolezaji waliohudhuria ibada maalum ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa kanisa Katoriki, papa  Benedict, iliyofanyika katika eneo la St. Peter.  


Ibada hiyo ya mazishi ya Benedict iliyohudhuriwa na makadinali 125, maaskofu 200 na wachungaji wapatao 3,700. Francis alizungumzia “busara, huruma na unyenyekevu uliouonyesha kwa miaka mingi”.

Amemtaja Benedict kwa jina lake mara moja tu, katika mstari wa mwisho aliposema, “ Benedict, rafiki mwaminifu wa Yesu, furaha itimie wakati utapapoisikia sauti yake , sasa na milele” .


Ibada hiyo ya mazishi iliendela mpaka jioni pia ilihudhuriwa na maelfu ya waumini ikiwajumuisha watumishi wa kanisa kutoka nchi mbalimbali duniani na baadhi ya wakuu wachache wa nchi.