Jumatano , 6th Jul , 2022

Watu zaidi ya elfu 3 wanategemea kupimwa na kupatiwa matibabu katika hospitali ya Jeshi hilo iliyopo mkoani Dodoma kwa kipindi cha siku 3 mfululizo bure ,ikiwa ni vita dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi Martin Otieno

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi Martin Otieno amesema ameyabainisha hayo leo Jijini Dodoma mara baada yakukutana na wataalamu wa afya za kibingwa kutoka Hospitali ya Jeshi na wafanyakazi.

Amesema watatoa huduma zote za upimaji bure kwa muda wa siku 3 kuanzia tarehe 29,30 na 31 kwa mwezi wa 7 katika kituo cha Afya Polisi Dodoma, kwakua ni sehemu yakurudisha huduma kwa jamii kama inavyoelekezwa na Serikali ili kuokoa maisha ya watu na kuokoa fedha kwani baadhi ya magonjwa hutumia gharama kubwa kuyatibu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya figo, afya ya akili, chanjo ya Uviko 19, utoaji wa damu salama,magonjwa mbalimbali ya binadamu  na wataalamu wa mambo yakijinsia watatoa huduma hiyo.

Huduma zote zitatolewa na wataalamu wa magonjwa ya kibingwa kutoka Hospitali kubwa za Serikali wakiongozwa na mabingwa kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa.