Jumatano , 26th Aug , 2015

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema kuwa litatoa tamko la jeshi hilo juu ya Chama cha Mapinduzi kuzidisha muda wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za chama hicho wiki iliyopita.

Kamishna wa operesheni mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Paul Chagonja

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa wadau wa uchaguzi leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Mafunzo na Operasheni wa Jeshi la Polisi CP Paul Chagonja amesema kuwa wanashughulikia suala hilo na muda ukifika watatoa tamko.

Ameongeza kuwa ili uchaguzi uwe wa Amani ni lazima watu wote watimize wajibu wao.

Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwakilishwa na Jaji Mstaafu John Mkwawa amevitaka vyama vya siasa kuzingatia maadili ya uchaguzi waliosaini ili kulinda amani na kuepusha migogoro na uvunjifu wa Amani.

Kwa upande wa mwakilishi toka chama cha ADC Mwanaisha Yemba amevitaka vyama vyenye vikundi vya ulinzi kuwapa sare na alama maalum walinzi wao ili watambuliwe na kila mtu ili wakifanya vujo iwe rahisi kutambulika.