Polisi Mwanza waua 8 kwa siku mbili

Ijumaa , 16th Nov , 2018

Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Jonathan Shana amethibitisha kuawa kwa watu 7 wanaosadikika kuwa ni majambazi, katika eneo la kishiri kwenye majibizano ya risasi na jeshi la polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Jonathan Shana.

Kamanda Jonathan Shana amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo wakati jeshi la polisi likifanya doria maalum mkoani humo.

Akizungumza na www.eatv.tv amesema ni kweli Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwadhibitti watu hao waliotajwa kuwa ni majambazi na kukamata silaha mbili za kivita.

Hilo tukio la Kishiri limetokea majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo, na majambazi wote wameuawa wakati wa mapigano ya kurushiana risasi na jeshi la polisi na katika mapigano hayo tumekamata silaha mbili za kivita na risasi zaidi ya 71 majambazi wote wameuawa.”

Juzi Jeshi la polisi Mkoani Mwanza lilifanikiwa kumuua mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Yusuph anayedhaniwa kuwa ni jambazi sugu ambae alikuwa akifanya uhalifu katika maeneo mbalimbali mkoani humo na kufanya kuwa na jumla ya idadi ya watu nane.