Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha SP Solomon Mwangamilo na askari wengine wakiwajulia hali wahanga wa ajali za bodaboda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo SP Solomon Mwangamilo, akiongozana na askari wa kikosi hicho amesema kuwa lengo la kufika katika hospitali hiyo ni kukusanya taarifa zao na kutoa pole kwa wahanga wa ajali ambapo amebainisha kuwa hospitali hiyo ni maarufu kwa kutibu wagonjwa waliopata madhara yatokanayo na ajali mbalimbali kwa kanda hiyo.
Naye Katibu wa waendesha pikipiki wilaya ya Arusha Hakimu Msemo, amebainisha kuwa wapo baadhi ya waendesha pikipiki ambao wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha wendesha bodaboda wilaya ya Arusha amesema wao kama viongozi wamejifunza na kusema kuwa wanakwenda kuwa waeleza namna ajali zinavyo waacha wananchi na madhara ya kudumu.