
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo,
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo, amesema basi hilo dogo la abiria lilikuwa likitoka Bagamoyo kuelekea mkoani Morogoro.
Lutumo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea Januari 8 mwaka huu majira ya saa 1:40 asubuhi na kwamba chanzo cha ajali ni basi dogo aina ya Coaster lilikuwa linapita gari lingine bila tahadhari na kugongana na gari lingine kusababisha ajali hiyo.