Alhamisi , 6th Oct , 2022

Jeshi la Polisi nchini limewataka wahitimu wa darasa la saba waliomaliza mitihani yao leo kote nchini Polisi kudumisha nidhamu, utii, kujitunza, kutojihusisha katika vitendo vya kihalifu kama vile uvutaji bangi, ulevi, uasherati, kuangalia picha za ngono

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Wahitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi Mlezi iliyopo jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mlezi Anicetus Lyimo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua zake za kuzungumza na wahitimu jambo ambalo litawafanya kutulia nyumbani na kutojiingiza katika vitendo viovu