
Eneo la ajali iliyouwa wafanyakazi wa TRA
Akizungumza hii leo Agosti 23, 2021, na EATV & East Africa Radio Digital, Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Janeth Magomi, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 11:45 alfajiri katika eneo la Hanseketwa- Old Vwawa.
Kamanda Magomi amesema kwamba ajali hiyo imesababisha vifo vya wafanyakazi wanne wa TRA mkoa wa Mbeya na mmoja wa TRA Tunduma, ambapo wote walikuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya doria mipakani kwa lengo la kukomesha biashara ya magendo.
Miili ya marehemu hao wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Songwe.