
Usafiri wa treni
Akizungumza na wanahabari mapema leo Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa amesema kuwa ujenzi huo utachukua muda wa miaka mitatu na utakuwa na upana wa mitaa 1.345, na kwamba treni hiyo itatembea kwa kasi ya Kilometa 120 kwa saa na itachukuwa jumla ya asilimia 60 ya mitandao ya reli katika dunia.
Aidha, amesema ujenzi utagawanywa katika awamu ndogo nne ambapo awamu ya kwanza itakuwa treni ya kutoka Dar hadi Morogoro ikiwa na kilometa 202, awamu ya pili itakuwa Morogoro hadi Makutupora yenye Kilometa 344.
Awamu ya tatu ni kutoka Makutupora hadi Tabora kwa kilometa 294 na awamu ya nne ni Tabora hadi Mwanza yenye kilometa 379, ambapo kiasi cha fedha kitakachotumika katika mradi huo akikuwekwa wazi.
Kadogosa amesema, Desemba mwaka huu mzabuni atakaye simamia ujenzi huo atatangazwa ili kuanza shuguli za ujenzi wa reli hiyo ya kisasa.