Rais afanya mabadiliko baraza la mawaziri

Jumatano , 15th Mei , 2019

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, amefanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri, kwa kumhamisha waziri wa Nishati Joram MacDonald Gumbo.

Joram MacDonald Gumbo

Gumbo ametolewa kwenye wizara hiyo kufuatia kuendelea kukumbwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, tangu mwaka 2016.

Nafasi ya Gumbo imechukuliwa na aliyekuwa Naibu waziri wa Usafirishaji na Maendeleo ya Miundombinu, Fortune Chasi.

Aidha Joram MacDonald Gumbo amehamishiwa Ofisi ya Rais, Mahusiano, Mipango na Usimamizi.