Rais Magufuli aeleza kuhusu uhuru wa Bunge

Jumatano , 6th Feb , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amebainisha kuwa katika kipindi cha utawala wake hataingilia uhuru wa mhimili wa Mahakama, na Bunge katika utekelezaji wa majukumu yao.

Rais Magufuli akipeana mkono na Spika Ndugai

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam alipokuwa kwenye uzinduzi wa Mahakama inayotembea ambapo amedai katika uongozi wake atahakikisha jambo hilo halitatokea kamwe.

"Mimi nimejitahidi sana katika uongozi wangu kutokuingilia muhimili wowote, sijaingilia Bunge hata wakizungumza kule wanakutukana sanasana unazima Tv, sijaingilia mahakama, ndiyo uhuru huo" - amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema, "kwa ndugu zangu wapelelezi, kapelelezeni haraka, mtu ameshikwa ameiba na kithibiti anacho labda hata amefungiwa nacho shingoni, bado unataka ukapeleleze tu, unataka ukapeleleza alivyoiba alikuwa ameinama au amesimama".