Jumatatu , 9th Dec , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, ametangaza kuwaachia wafungwa 5533 ambao walikuwa wamefungwa katika Magereza mbalimbali nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho wa miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambapo kuna idadi kubwa ya wafungwa ambao wapo Magerezani kwa makosa ya kawaida sana.

"Nilitembelea Magereza nikashuhudia kuna mlundikano wa wafungwa, mpaka leo kuna Wafungwa 17,547 na Mahabusu 18,256, hii ni idadi kubwa, kwa hao wafungwa kuna baadhi wamefungwa makosa madogo, sijui kaiba Kuku, kujibizana na mpenzi wake" amesema Rais Magufuli

"Hali ya pale Butimba ilinihuzunisha sana, kwa kutambua Dini zote zinatufundisha tusamehe na kuamini wafungwa wengi wanajutia makosa yao, kwa mujibu wa Mamlaka niliyonayo ya Kikatiba, nimewasamehe wafungwa 5533" ameongeza Rais Magufuli