
Rais Dkt. John Magufuli
Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wabunge wa chama hicho siku kadhaa zilizopita, katika video iliyochapishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Rais Magufuli amesema kuwa lazima watu waridhike kwani hawawezi kuwa na vyote.
"Hao wanaojipanga kugombea uchaguzi ujao wakiwemo wakurugenzi, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa nyie waacheni tu, wakagombee nyie fanyeni kazi, kuna watu wanatamaa sana", amesema Rais Magufuli.
Akitolea mfano wa baadhi ya viongozi waliowahi kutumikia nyadhifa za ukuu wa mkoa na wilaya na baadaye kugombea nafasi za ubunge, Rais Magufuli amesema kuwa sio kwamba hawaoni au hawafahamu bali ameona wanatamaa na hawamfai katika serikali yake.
Bofya link hapo chini kumtazama Rais Magufuli akizungumza.