
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mtwara Mohamed Sinani.
Akizungumza baada ya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama, amesema mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo ulianza miaka 40 iliyopita na kwamba mpaka sasa haujakamilika.
Sinani amesema kuwa kwa sasa kuna umuhimu wa kumalizika kwa hospitali hiyo kwa haraka zaidi kwa kuwa mahitaji ya huduma za afya yanatakiwa kuongezeka mkoani huo kutokana na ongezeko la watu na ukuaji wa kasi wa mkoa huo.
Jumla ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 75 zimetengwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa hospitali.