
Ruto amesema amekuwa akimtafuta kiongozi huyo wa chama cha Wiper ili ampe majukumu ya kiserikali
“Nipo tayari kufanya kazi na Kalonzo wakati wowote ule, atakapokuwa tayari,” amesema Ruto.
Musyoka alikuwa makamu wa rais wakati wa utawala wa hayati Mwai Kibaki na amewahi kuwa waziri wa mazingira, mambo ya nje na elimu chini ya utawala wa hayati Daniel Arap Moi