
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Aidha Rais Samia amewateua Maofisa watano (05) kuwa Wajumbe wa Bodi ya DART.
Pia amemteua Bi. Beng’i Mazana Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya mikopo ya serikali za mitaa, na Bi. Beng’i ni Katibu Mtendaji, baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).
Katika hatua nyingine Rais Samia amemteua Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Mganga Mkuu wa Serikali na kabla ya uteuzi huu Prof. Nagu alikuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Tiba, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Prof. Nagu anachukua nafasi ya Dkt. Aifello Sichalwe ambaye atapangiwa kazi nyingine na uteuzi wa Prof. Nagu umeanza Oktoba 19, 2022.