Alhamisi , 30th Sep , 2021

Rais Samia ameshiriki ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Tate Ole Nasha, iliyofanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Tate Ole Nasha

Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, ametoa pole kwa familia pamoja na kwa Rais Samia kwa kumpoteza Naibu Waziri mchapakazi na aliyefanya kazi yake kwa uzalendo mkubwa.

Ole Nasha alifariki dunia Septemba 27, 2021 akiwa nyumbani kwake mtaa wa Medeli jijini Dodoma na mwili wake unatarajia kusafirishwa kesho Ijumaa Oktoba Mosi, 2021  kwenda Ngorongoro na  mazishi yatafanyika Jumamosi Oktoba 2 mwaka huu.