
Rais Dkt. Ali Mohamed Shein akitazama meli ya MT MKOMBOZI II wakati ikiwasili kwenye bandari ya Malindi.
Ahadi hiyo imekamilika leo Agosti 7, 2019, mara baada ya meli hiyo kuwasili katika bandari ya Zanziba ikitokea Shanghai nchini China.
Meli ya MT MKOMBOZI II iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyard ya nchini Uholanzi, imewasili rasmi katika Bandari ya Malindi Zanzibar majira ya asubuhi na kupata mapokezi ya aina yake.
Meli hiyo ilianzwa kutengenezwa Julai 2018 na kumalizika mwezi April 2019 na imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36.