
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte
Duterte alikuwa Meya wa mji huo kwa miongo miwili na kupewa sifa za kuudhibiti uhalifu na kutuhumiwa kwa kuunga mkono kuwepo kwa kikosi cha mauwaji.
Rais Duterte alikuwa akiongea na viongozi wa kibiashara Ufilipino siku ya Jumatatu kabla ya safari yake ya kwenda nje ya nchi.
Kauli hiyo ni mfululizo wa kauli tata ambazo amekuwa akitoa kiongozi huyo.
Rais huyo amekaririwa akisema kwamba alikuwa akiendesha pikipiki usiku akitafuta mahali zilipo vurugu ambako angemuua mtuhumiwa,kauli inayoridhia kuwa askari polisi wanaweweza kufanya hivyo.