Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa hii leo Februari 24, 2023, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, ambapo pia Rais Samia amemteua Mussa Mohammed Makame kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), ambapo Kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC pamoja na Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini na amechukua nafasi ya James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha Rais Samia amemteua Hamad Abdallah kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), na kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Nehemia Mchechu, ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.



