Jumamosi , 24th Jul , 2021

Aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa Kilimanjaro Band maarufu kama Njenje Waziri Ally amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala.

Waziri Ally wakati wa uhai wake

Taarifa kamili kuhusu raitba ya mazishi yake iliyotolewa na Aboubakary Liongo kwa niaba ya familia inaeleza kuwa.

"Ndugu na jamaa wote kukutana Mwananyamala Hospitali  asubuhi hii, tunatarajia mwili utasafirishwa leo saa tano asubuhi kwenda Tanga ambako msiba utakuwa barabara ya 21 karibu na kiwanda cha Chuma zamani na mazishi yatakuwa kesho Jumapili kijijini kwao Pongwe".