
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge (kushoto) alipotembelea ofisi za East Africa Television na East Africa Radio na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji Regina Mengi (kulia).
RC Kunenge ameainisha mikakati hiyo leo Januari 7, 2021, katika ziara yake katika vyombo vya habari vya IPP Media, na kutaja mmoja wa mkakati wanaofanya ni kuwatambua akina mama na kuwawezesha ili waweze kuinua jamii licha ya makao makuu kuhamia Dodoma amesema jiji la Dar ni maarufu kwa biashara.
“Mikakati yetu ni kuhakikisha tunakuza biashara za mji huu katika nchi jirani na kutoa mikopp kwa akina mama ambayo inatokana na mapato ndani ya Halmashauri, kwa akina mama wanaoanza chini tunawapatia mafunzo na tunajaribu kuondoa urasimu kwenye vibali vya kufanya biashara ili wafanyabiashara wadogo wasiweze kusumbuliwa”, - amesema Kunenge.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mh. Aboubakar Mussa Kunenge akiwa na wafanyakazi wa East Africa Television na East Africa Radio.
Katika ziara hiyo RC Kunenge ameitaja sababu ya kuahirisha kikao chake na wafanyabiashara mkoani humu, kuwa waliahirisha ili kuhakikisha pale watakapofanya kikao hicho wanakuwa na majibu ya maswali yao ili kutatua matatizo.
Aidha amesema kwasasa hivi wameamua bAdala ya kutoa pesa kwa ajili ya kusaidia vikundi vya wajasiriamali au wafanyaboiashara, wanatoa vifaa na kuwapa mafunzo ambapo kwa mujibu wa tathmini walizofanya soko lipo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mh. Aboubakar Mussa Kunenge akipewa maelezo na Mratibu wa Vipindi East Africa Television Sophia Proches (kulia).
“Sisi sasa hivi tumeona badala yakutoa pesa tutoe vifaa kwa manispaa zote za Dare s salaam, na mbinu hii inatumika kwa manispaa hadi za mikoani, tunafuata vikundi vile tunavipa vifaa tulivyonunua na inasaidia sana kwasababu wengi ukiwapa pesa wanagawana”, ameeleza.
Tazama Video hapo chini