
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto.
Hayo ameyabainisha leo Aprili, 23, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa kwa sasa Serikali imepiga marufuku mikusanyiko ya watu wengi na kwamba hatua hizo walizichukua kwa lengo la kuwalinda wote kwa pamoja.
"Sababu kubwa alikuwa anafanya mikusanyiko ndani ya ofisi zake, tulikuwa tunainusuru hali yake ya kiafya na waandishi wetu wa habari, kwanza walishatuhumiwa na familia yake kama wana maambukizi na kama alikuwa na jambo la msingi la kuliambia Taifa angeenda Bungeni, mikusanyiko ni marufuku" amesema Kamanda Muroto.
Jana Aprili 22, 2020, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, alikuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo jijini Dodoma, lakini baadaye Jeshi la Polisi lilifika kwenye ofisi hizo na kuzuia mkutano huo.