Jumatatu , 5th Sep , 2022

Mahakama kuu nchini Kenya imemhidhinisha William Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya baada ya kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa Raila Odinga

Jaji Martha Koome wa mahakama hiyo akisoma hukumu hiyo amesema hakuna ushahidi wa moja kuwa moja unaoweza kubatilisha matokeo ya uchaguzi huo 

Mahakama hiyo imesema hakuna  ushahidi unaoonesha kwamba mfumo wa kuhesabu matokeo nchini humo uliingiliwa na mahakama haijashawishika kwamba viwango vya teknolojia ya IEBC vilifeli  na kwamba fomu zilizohitajika 32A zilijazwa kwa mafanikio

Aidha hakuna ushahidi wowote kwamba Tume ya uchaguzi ilifanya makusudi kuahirisha uchaguzi katika baadhi ya maeneo ili kumkandamiza Raila Odinga

Upande wa Raila Odinga uliwasilisha hoja tisa za kupinga matokeo ya uchaguzi huo na mahakama imesema nyingi zilikuwa hazina ukweli