
Kushoto ni Rais Uhuru Kenyatta, na kulia William Ruto
Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 31, 2022, wakati akifungua rasmi matumizi ya barabara za juu za Nairobi Expressway.
"Hakuna haja ya kuwaambia watu nataka kukuua, mmenitusi karibu miaka mitatu, kuna mtu amewagusa, si nilikuwa na uwezo, sasa sina uwezo ndiyo niko na time ya kukutafuta, piga story uza sera yako achana na mimi, mimi nafanya kazi yangu nimalize, nyie ombeni kura wananchi wakiwapatia sawa, wakiwanyima twende nyumbani pamoja, shida iko wapi si dunia itaendelea," amesema Rais Kenyatta.