
Serikali ya Rwanda imesema jana kwamba Kongo inayatengeneza mauaji hayo ya Kishishe ikiyaita ni uzushi unaoenea kwa haraka bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na taasisi yoyote ya kuaminika na kuongeza kuwa tukio hilo lilihusisha makabiliano kati ya wanamgambo wa M23 na makundi haramu yenye silaha yanayoshirikiana na jeshi la Kongo.
Imesema si haki kuituhumu Rwanda kwamba inawasidia M23 kwani hatua hiyo inalenga kuvuruga chanzo halisi cha kuendelea kwa mzozo mashariki mwa Kongo.
M23 inakana kuwa nyuma ya mauaji hayo ikisema ni raia wanane tu ambao iliwaua kwa bahati mbaya.