Akizungumza wakati wa kuwasainisha mikataba maafisa elimu wote wa mkoa wa Kagera inayolenga kuinua kiwanago cha ufaulu, katibu tawala wa mkoa Toba Nguvila amesema kuwa amefanya utafiti mdogo na kubaini kuwa shule nyingi zimekuwa hazimalizi mada mapema kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo uwajiikaji duni wa wataalamu
"Unakuta mtoto badala ya kuwa amemaliza mada (syllabus) sita kamaliza tatu, na mtihani ukitungwa unajumuisha mada zote, kwa hiyo unakuta ana uwezo wa mada hizo alizofundishwa tu, hawezi kufanya vizuri katika mitihani, sasa tunakwenda kufanya mashindano ya kulindoa hili lengo mtoto akiingia katika mitihani awe na umahiri katika mada zote, mnapokwenda huko lazima muwasimamie walimu na kuwafuatilia" amesema.
Aidha amesema kuwa pia wanakwenda kuanza mitihani katika mkoa ambayo utakuwa mmoja kila somo, na kuwataka maafisa elimu kuwateua walimu mahiri kuandaa mitihani hiyo, ili kuepuka watoto kutungiwa mitihani myepesi wakaona wana uwezo mkubwa na baadae kushindwa kufaulu mitihani ya taifa.
"Kuna walimu wanaona watoto wanafanya vizuri katika masomo yao, lakini kumbe wanatunga mitihani myepesi tena ambayo haigusi mada zote, matokeo yake wanafeli mitihani ya taifa" amesema Nguvila.
