
Kushoto ni Dkt. Sospeter Bulugu, aliyetetemeka wakati wa mdahalo na kulia ni Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima
Juzi Agosti 12, 2021, wakati mdahalo huo ukiendelea Dkt. Sospeter Bulugu, alishindwa kuwasilisha mada yake baada ya kupata kizunguzungu kilichotokana na sukari kwenye damu kushuka, na kwamba Watanzania wametakiwa kupuuza uzushi huo kuwa alitetemeka kutokana na madhara ya chanjo ya COVID-19.
Aidha, Dkt. Sichwale ameeleza kuwa madai ya kuwa Waziri wa Afya, alitaka kuficha jambo kuhusu madhara ya chanjo si ya kweli kwani kuvitaka vyombo vya habari visichukue tukio hilo yeye alikuwa akitekeleza majukumu yake ya maadili ya kitaaluma pale panapokuwa na mteja anayepokea huduma ambaye hajaridhia kwa hiari yake kwamba huduma hiyo iwe wazi.
Dkt. Sichwale ameongeza kuwa hata hivyo Dkt. Bulugu aliyekutwa na changamoto hiyo hajawahi kupata chanjo ya COVID-19.