Ijumaa , 16th Nov , 2018

Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini, Alex Kimbe amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia a Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kwa tuhuma za kupokea rushwa ambapo ni kinyume na sheria za makosa ya jinai nchini

Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini, Alex Kimbe.

Taarifa za kukamatwa kwa Meya huyo zilianza kusambaa jana kupitia mitandao ya kijamii, zikimtaja Meya huyo kuwa alikuwa kwenye moja ya hoteli mjini Iringa, ambapo alikutwa na fedha hizo baada ya kuwekewa kwa mtego.

Akizungumza na www.eatv.tv Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Peter Msigwa amethibitisha kukamatwa kwa Meya wake wa Manispaa ya Iringa ambapo amesema "ni kweli kiongozi (Meya) amekamatwa na mimi niko Dodoma nitahakikisha mpaka mchana nalifuatilia suala hilo".

Meya Alex Kimbe amekuwa akiingia kwenye migogoro ya mara kwa mara na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi kutokana na sababu mbalimbali za kiutawala, ambapo hivi karibuni alinukuliwa akimtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuomba radhi

Kwa kiongozi mzuri anapaswa ajitafakari, kama Waziri ameomba radhi kwa niaba yake yeye pia Mkuu wa Mkoa aombe radhi, lakini pia unakumbuka mambo yaleyale ambayo sisi tuliyasema kwamba anakiuka sheria”, Alex Kimbe.