Sabaya arejesha eneo liliporwa na Kapteni Mstaafu

Jumatatu , 2nd Dec , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amerejesha eneo lenye ukubwa wa Ekari mbili, mali ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wilayani humo, lililokuwa limeporwa na Kapteni Mstaafu wa JWTZ, John Mushi kwa takribani miaka 35.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akizungumza na Capt, Mstaafu wa JWTZ wilayani humo, John Mushi.

Eneo hilo amelirejesha leo Desemba 2, 2019, na kuwaagiza TAKUKURU kuwa wahakikishe anazilipa fedha zote za Serikali na kwamba mtuhumiwa huyo amekuwa akitoa kauli za vitisho kwa maafisa wa Serikali, waliokuwa wakifika katika eneo hilo kwa lengo la kujua umiliki halali wa eneo hilo. 

Inadaiwa kuwa Kapteni huyo Mstaafu wa Wilaya hiyo alikuwa akimiliki eneo hilo kwa mabavu bila kulipa kodi ya ardhi, kiasi cha Shilingi milioni 20 na kulikodisha eneo hilo kwa mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi.