
Kupima Ukimwi
kupima Ukimwi bila ridhaa ya mzazi.
Muswada huo umepitishwa leo Novemba 12, 2019, ambao utasaidia watu kujitambua hali zao mapema, hususani wanaume na kundi la vijana, ambalo kwa sasa ndilo linaloongoza kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo.
Akizungumza bungeni Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile, amesema kuwa tayari Wizara imekwishajipanga juu ya upatikanaji wa vipimo hivyo na tayari imeshaanza kufanya majaribio ya mifumo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia mapokea kutoka kwa wananchi.
"Vipimo hivi havitakuwa vinatumia damu, vitakuwa vinatumia sampuli ya kinywa na hii watu watapima hata kabla ya kujamiiana na watakapobaini wamepata changamoto hizo wanakuja katika vituo vya kutoa huduma za afya ili kujiridhisha,vijana wengi wameanza kuathirika na kujamiiana wakiwa na umri mdogo, sasa tunatoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kupima Ukimwi bila ridhaa ya mzazi wake" amesema Waziri Dkt Ndugulile.