Ijumaa , 15th Aug , 2025

Maandamano ya kuipinga serikali ya Serbia yamerejea tena baada ya juhudi za majadiliano kugonga mwamba

Maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali walirejea mitaani nchini Serbia hapo jana baada ya siku mbili za makabiliano na wafuasi wa Rais Aleksandar Vucic na polisi wa kutuliza ghasia ambayo yamesababisha makumi ya watu kujeruhiwa au kushikiliwa.

Polisi walifyatua mabomu ya kutowa machozi katika miji miwili huku matukio kadha ya ghasia yakiripotiwa. Katika mji wa kaskazini wa Novi Sad ambako maandamano ya kumpinga Vucic yalianzia, makundi ya waandamanaji yalivunja ofisi za chama tawala cha Serbia Progressive Party.

Rais Vucic ameapa kukabiliana na waandamanaji wanaoipinga serikali, akiwashutumu kwa kuchochea ghasia na kuwa maadui wa nchi.

Maandamano yalizuka Novembabaada ya dari katika kituo cha treni kilichokarabatiwa kuanguka huko Novi Sad na kuua watu 16 na kuzusha tuhuma za ufisadi katika miradi ya miundombinu ya serikali