Jumatatu , 27th Jun , 2022

Naibu Waziri wa Elimu Dkt. Omary Kipanga, amesema kwamba kutokana na kwamba mazingira ya Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS), kuwa madogo na yaliyobana, serikali imejipanga kujenga kampasi zingine za vyuo hivyo katika eneo la Mloganzila, mkoani Kigoma na Mbeya.

Naibu Waziri wa Elimu Dkt. Omary Kipanga

Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 27, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la mbunge Dkt. Nahato, aliyehoji mpango wa serikali katika kukipanua chuo hicho.

"Tunakwenda kufanya mageuzi makubwa katika chuo chetu cha Muhimbili kwa kujenga Chuo Kikuu kipya katika eneo la Mloganzila, tunafungua kampasi nyingine mpya mkoa wa Kigoma na Mbeya, mchakato umeshaanza na tutadahili wanafunzi wa kutosha kuhakikisha kwamba tunapata wataalam wa tiba hapa nchini," amesema Naibu Waziri.