Jumatano , 11th Mei , 2016

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba amesema serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa utaratibu maalum, kujishughulisha na kilimo hususanI vijana watakaonyesha muamko na kilimo kwa kupata mbegu bora ili kuongeza uzalishaji nchini.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba.

Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma wakati kipindi cha Maswali na Majibu, Mhe. Nchemba amesema kuwa ameshawaagiza wataalamu wake wampe mashamba yote ambayo yalishageuka kama mapori ili kutengeneza ushirika wa vijana wanaotaka kujihusisha kwenye Kilimo.

Mhe. Mwigulu amesema licha ya kufanya hivyo lakini zoezi hilo halitakua endelevu kutokana na kuwa vijana ni wengi kuliko ardhi inayotaka kugawiwa hivyo, serikali itaweka vijana kwenye vikundi ili kutimiza lengo la uzalishaji na kukuza uchumi kupita vijana.

Mhe. Mwigulu alitoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa kutokana na baadhi ya wabunge wa Mbeya akiwemo mbunge wa Mbozi na Vwawa waliotaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwagawia wananchi mashamba ambayo hayaendelezwi na kubaki mapori.

Sauti ya Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba.