Jumamosi , 30th Mar , 2019

Serikali imetangaza mpango wa ujenzi wa mradi mkubwa wa daraja ambao utaleta mageuzi makubwa katika sekta ya usafriri nchini lakini haijataja ni wapi utajengwa na ni lini utaanza ujenzi rasmi.

Mradi mpya uliotangazwa na serikali

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dakt Hassan Abasi kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo ameuita mradi huo kuwa ni utekelezaji wa mageuzi ya kaulimbiu ya 'TUNATEKELEZA2019'.

Mradi huo mkubwa wa daraja utakuwa ni wa pili, baada ya ule wa Daraja la Nyerere ambao umejengwa Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam na kugharimu takribani Shilingi bilioni 300.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.