
Haji Manara
Mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro, Simba inazisaka pointi tatu ili kuikimbiza Yanga iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika ujumbe akisema kuwa, "kikosi cha kisasi!. Mbao mtatusamehe kwa kesho, saa mbaya hz!, kipute hiki ni Jumapili ya kesho Jamhuri Stadium Morogoro Saa kumi alasiri".
Katika msimamo wa Ligi Kuu, Simba inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 baada ya kushuka dimbani michezo 21 huku Mbao FC ikiwa katika nafasi ya 14 kwa pointi 36 baada ya kushuka dimbani michezo 30.
Endapo Simba itaibuka na ushindi katika mchezo wa leo, itafikisha jumla ya michezo 10 mfululizo ya ushindi katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Itaweka historia kwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kushinda michezo 10 mfululizo.
Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.