Ijumaa , 22nd Jul , 2016

Serikali ya Tanzania imesema kuwa imeandaa mpango maalum wa upimaji wa ardhi na urasimishaji wa maeneo yote yasiyopimwa katika jiji la Dar es Salaam ambapo viwanja zaidi ya laki tatu vitapimwa na wamiliki kupewa hati.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka,

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam, kuhusu mpango huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka, amesema kuwa serikali imeamua kuja na mpango huo kwa sababu ya ukubwa wa jiji na wingi wa watu pamoja na ujenzi holela.

Dkt. Kusiluka masema kuwa baada ya mapango wa uhakiki,serikali itatoa hati za maeneo hayo na kusisitiza kuwa kazi hiyo wataifanya pia katika maeneo mengine ya miji mikubwa ikiwemo Mwanza na Arusha.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa urasimishaji huo utakuwa shirikishi kwa kuwahusisha watu wote wa maeneo yatakayopimwa na serikali ambapo wananchi wenye nyumba watashirikiana na viongozi wa serikali.

Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria zinazosimamia Sekta ya Ardhi nchini,bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya wakulima na wafugaji,migogoro ya kijinai, migogoro ya mipaka na mengineyo.