Jumatatu , 7th Nov , 2016

Serikali imekiri uwepo wa upungu wa watumishi wa afya kwa asilimia 48 kwa nchi nzima hivyo kuanza mikakati ya kutoa ajira katika sekta hiyo ili kuweza kuwapangia katika maeneo yenye upungufu ili kuboresha sekta hiyo muhimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

 

Akiongea leo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa licha kufanya hivyo lakini pia serikali itamalizia vituo vya afya na Zahanati ambazo hazijaisha ili kutatua changamoto ya ukosefu wa vituo hivyo.

Mhe. Mwalimu ametumia fursa hiyo pia kuwataka makatibu tawala wote nchi nzima kupanga kuwapanga upya wataalamu wa afya walionao katika maeneo mbalimbali badala ya kuwaacha wakirundikana katika eneo moja huku vituo vikikosa wataalamu hao.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa tayari wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya TAMISEMI wameshafanya tathmini ya vituo vya afya kwa ajili ya kufanyika ukarabati ili hadi kufikia 2018 wawe wamejenga vituo vya afya zaidi ya mia tano kwa nchi nzima.