Shambulio lingine latokea Kenya, 6 wauawa

Jumanne , 7th Jan , 2020

Watu 6 wakiwemo wanaodaiwa kuwa ni Magaidi 2 wameuawa katika eneo la Saretho , Garissa, nchini Kenya baada ya Magaidi kujaribu kuvamia Kituo cha Polisi Daadab.

Wanajeshi wa Kenya.

Katika Watu 6 hao waliouawa watu wawili wanadaiwa kuwa Magaidi, yumo mtoto ambaye ni mwanafunzi na Mwalimu wake ambapo tukio limetokea alfajiri ya leo eneo la Saretho Kaunti ya Garisa, kutoka Kambi ya Wakimbizi ya Daadab.

Kwa mujibu wa Polisi katika tukio hilo wamekamata Bunduki aina ya AK 47, ambapo pia wamekamata mabomu kutoka Magaidi.

Hili ni shambulio la tatu chini ya wiki moja.