Jumatatu , 10th Oct , 2022

Shirika la Posta Tanzania Sumbawanga  Mkoani Rukwa, limetoa msaada wa wa vyakula na mafuta kwa watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma  shule ya Msingi Malamngali, inayohudumia watoto wenye mahitaji maalum ikiwa ni juhudi za kuhakikisha wanapata huduma stahiki na afya bora.

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja Shirika la Posta Sumbawanga limeeleza faida waliyoipata kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Shule Maalum ya Msingi Malamngali inahudumia zaidi ya watoto 90 wenye mahitaji maalum lakini ufinyu wa bajeti  unaelezwa kuwa kikwazo Katika kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanayafikia malengo yao.