Waziri Mkuu ameyasema hayo leo bungeni baada ya Mbunge wa Viti maalum Chadema Kunti Majala kuuliza swali kwamba kuna mikataba ambayo inatekelezwa nchini na serikali wakati bunge halikupitisha mikataba hiyo.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Majaliwa amesema kwamba kama bunge lingekuwa linapelekewa mikataba yote basi lingefanya kazi ya kushughulika na mikataba tuu.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaruhusiwa kusaini mikataba ya nchi kwa niaba ya serikali hivyo hakuna kosa lolote serikali imefanya kwa kutopeleka mikataba hiyo bungeni.
Bunge la 11 mkutano wa tatu kikao cha saba limeendelea leo ambapo serikali imeweza kutoa majibu ya maswali kwa wabunge kutoka maeneo mbalimbali.





