Hasina anatuhumiwa kuwa nyuma ya mamia ya mauaji wakati wa maandamano makubwa ya kupinga utawala wake wa kiimla - madai ambayo anayakanusha.
Amesema kesi yake bila kuwepo mahakamani ilikuwa "ujinga" uliopangwa na "mahakama isiyo na haki" inayodhibitiwa na wapinzani wa kisiasa.
Waendesha mashtaka wanatafuta hukumu ya kifo kwa Hasina iwapo atapatikana na hatia siku ya Jumatatu.
