Silaha zaibiwa kituo cha polisi

Jumatano , 17th Apr , 2019

Wezi wamevunja kituo cha polisi cha Kamorwon kilichopo kaunti ya Nandi nchini Kenya, na kuiba baadhi ya silaha zilikuwepo katika kituo hicho.

Taarifa kutoka Kenya ambazo zimechapishwa na jarida la Standard Digital zinasema kwamba wakati wezi hao wakifanya uhalifu kwenye kituo cha polisi, askari waliokuwepo zamu walikuwa wanaangalia mpira, sehemu ya jirani na kituo hicho., siku ya Jumanne ya April 16.

Jinsi walivyogundua silaha zimeibiwa

 

Baada ya kurudi kituoni hapo waligundua chumba cha askari wa zamu ambacho ndicho kiliwekwa silaha kipo wazi, huku sanduku la chuma ambalo huwekwa silaha likiwa limevunjwa.

Wezi hao wameiba silaha aina ya rifle pamoja na magazine zenye uwezo wa kuweka risasi 20, na kuacha magazine 2 zenye uwezo wa kubeba risasi 17 hadi 20.

Uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea huku ikielezwa kwamba Mkuu wa Polisi eneo la Nandi,  OCPD, OCS na AP Kamanda, kufika eneo la tukio kushuhudia jinsi tukio hilo.