Waziri atoa sababu jengo la wizara kuchelewa

Jumatano , 17th Apr , 2019

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameweka wazi sababu zilizochangia kuchelewashwa kwa ujenzi wa jengo jipya la wizara yake jiini Dodoma, na kupelekea kuhamia kwenye mabati.

Waziri atoa maelezo zaidi

 

Akizungumzia hilo, Waziri Jafo amesema kwamba jengo hilo limechelewa kutokana na utaalamu uliotumika kulijenga kuchukua muda mrefu, kwani walifanya vipimo vya kisayansi ili kuweka uimara na ubora zaidi, kutokana na asili ya maeneo hayo kuwa na tatizo la kijiografia.

“Kama unavyoona hapa sasa linaeleka mwisho, jengo hili lilichelewa kwa sababu ni jengo pekee ambalo lilifanyika geological analysis, kwa ajili ya kuhakikisha nature haiharibu, nikasema mimi kama Waziri siwezi nikajenga jengo hapa, lazima tuzingatie vigezo, wenzetu wa TBA tukashirikiana ikafanyika Geological analysis, ikachukua muda kidogo lakini baadaye ikatuonesha foundation yake iundwe chini, ili kuhakikisha uimara wa hili jengo”, amesema Waziri Jafo.

Mapema Wiki hii wafanyakazi wa wizara hiyo walitakiwa kuhamia Dodoma licha ya jengo lao la Wizara kutokamilika, jambo lililowalazimu kuhamia kwenye ofisi zilizojengwa kwa mabati.

Jengo la mabati ambalo Waziri amehamia